JIFUNZE KUMVUTA MTEJA BILA KUTUMIA NGUVU NA GHARAMA KUBWA
Mteja anastahili kuthaminiwa sio kwa sababu ya jinsi alivyo ila ni kwa sababu ya kile anachokileta kwenye biashara yako yaani fedha.
Hakuna biashara nzuri inayomzidi uzuri mteja simaanishi uzuri wa muonekano, namaanisha kile ambacho kinaifanya biashara iwe nzuri ambacho hakitoki kwa mfanyabiashara ila ni kwa mteja.
Kamwe usibebe dhana kwamba una biashara kubwa kuzidi ukubwa wa pesa unayoitaka kutoka kwa wateja. Usidhani kwamba pesa uliyowekeza kama mtaji ni kubwa kuliko faida ambayo unaitaka kutoka kwa wateja.
Mteja sio tu mfalme anayepaswa kusujudiwa, mteja ni uzima wa biashara ambaye anapaswa kutunzwa kwa umakini na uangalifu mkubwa ili asitetereke na kuyumbisha biashara.
Kamwe usimuwekee mteja masharti magumu au kumtaka atii au aendane na itikadi, misimamo, mlengo, mtazamo na imani yako ambayo kwake haimuongezei chochote ila kwako inakuathiri.
Acha kutumia biashara kama eneo la kugawa watu badala yake fanya eneo la biashara yako kuwa kama kituo cha kufufua matumaini na chanzo cha maambukizi ya tabasamu kwa kuwa na huduma nzuri na hivyo ndivyo ambavyo wateja wanarogwa na kufanywa kuwa wa kudumu kwenye biashara.
___________________
Kwa elimu zaidi soma kitabu cha NAMNA YA KUIFANYA BI’HASARA KUWA BIASHARA INAYOLIPA au ELIMU YA BI’FAIDA KATIKA MASOKO NA MAUZO kwa Sh. 5000/= kwa kitabu kimoja.
Lipia kitabu chako kuja namba 0620 443 048 jina Victor Ramadhan Kalinga kisha nijulishe ili nikutumie kitabu chako kwa WhatsApp au Email.
ByChankysupply
Leave a Comment