MWANAUME USINUNUE NGOโMBE KIJIJI ULICHOPO:
โโโโโโโโโโโโโโโโโโโ
Mwanaume, unaponunua ngoโmbe kamwe usinunue kwenye eneo au kijiji ulichopo. Kwanini?! Kwa sababu kuna siku ngโombe ataenda mtoni kwa lengo la kunywa maji.
Kisia nani atakuwa eneo hilo?! Ni mmiliki wake wa mwanzoni. Unajua atakachokifanya huyo mmiliki wake wa zamani?!
Atakachofanya ni kumpigia mluzi, na ngโombe atatambua mluzi wa mmiliki wake wa zamani. Atamfuata. Ngโombe atakapomfuata mmiliki wake wa zamani, kitakachofuata ni zoezi la kukamuliwa maziwa yote mazuri.
Baada ya hapo mmiliki wa zamani atampa pasa papasa ngโombe juu ya mgongo. Na kumuacha aondoke kana kwamba hakuna lolote lililotokea.
Kisha wewe mmiliki mpya ukimuona ngโombe karudi nyumbani. Utajawa furaha na kuchukua ndoo ndogo ukitaka umkamue maziwa fresh.
Lakini ngโombe atakuwa mkali, atakupa Kung Fu kick moja takatifu. Huku akitoa mlio wa hasira. Sababu ngโombe huwa hapendi utaratibu wa kukamuliwa maziwa yake mara kwa mara tena kwa siku nzi